Afrika Kusini yaruhusu biashara ya pembe za Faru
Wakati Tanzania pamoja na nchi za Afrika Mashariki zikipambana na
biashara ya pembe za faru, Mahakama ya katiba ya Afrika kusini
imelipinga jaribio la serikali la kutaka kuweka marufuku kwa biashara ya
pembe za faru katika matumizi ya ndani.
Matokeo yake ni kwamba pembe hizo za faru zinaweza kuuzwa ndani ya
nchi huku marufuku katika biashara hiyo kimataifa ikiwa bado inaendelea.
Watunzaji wa wanyama pori hao wamedai kuwa, kuruhusu biashara hiyo kuendelea kufanyika kihalali kutaweza kupunguza idadi ya faru wanaouwawa kutokana na kwamba pembe za faru zinaweza kukatwa na kuacha wanyama hao hai.
Hata hivyo wahifadhi wa wanyama pori hawakubaliani na hatua hiyo.

No comments: