Bahati asimulia kilichomtokea kwa Lulu
Mapenzi ya Bahati kwa Elizabeth ‘Lulu’ Michael yalimtokea puani.
Muimbaji huyo wa gospel amefunguka kuwa aliwahi kuja Bongo kwa ajili
ya kumpata mrembo huyo wa filamu nchini ili amweke kwenye video ya wimbo
wake ‘Maria’ lakini ilishindikana ndipo alipoamua kumtumia Jokate kama
model kwenye video hiyo.
“Hii ni siri ambayo nadhani hata Wakenya hawakujua, AY peke yake ndiye alijua. Nilitoka Nairobi kuja hapa [Dar es Salaam] natafuta connection na Lulu kwasababu nataka awe kwenye ile video [Maria] ambayo nimemweka Jokate. Nimekaa kwa hotel Lulu amekataa kushika simu mpaka ikafika mahali nikamwambia ukija kuniona Mungu atakubariki, siku ya pili akakataa kabisa nikamwambia mshikaji AY acha tu nirudi nyumbani. Nikarudi hivyo,” Bahati amesema hayo kupitia Magic FM.
Bahati ameongeza kuwa sababu ya kufanya kazi na Ray Vanny katika wimbo wao mpya ‘Nikumbushe’ ilikuwa ni mipango yake ya muda mrefu ili muziki wake uweze kupata tobo hapa nchini.

No comments: