Askofu Gwajima kuzuru IPP Media Ijumaa hii
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Bishop Josephat Gwajima amesema
kuwa Ijumaa hii atatembelea IPP media kwaajili ya kuwapa pole wana
tasnia ya habari kwa yaliyotokea.
Ijumaa iliyopita kituo cha Clouds kilivamiwa na Mkuu wa mkoa wa Dar
es Salaam, Paul Makonda akiwa na askari wenye mitutu kitendo
kilichopingwa na wadau mbalimbali wa habari.
“Kesho 24/03/2017 nitatembelea ofisi za IPP Media ikiwa ni ziara Ya kuwapa pole wanatasnia ya Habari kwa yaliyotokea,” ameandika kupitia akaunti yake ya Instagram.
Alhamisi hii Askofu huyo ametembelea EFM redio na TVE.

No comments: