Hiki ndicho kilichoandikwa na Zitto na Nay baada ya Roma na Moni kutekwa
Kitendo cha rapper Roma Mkatoliki na Moni Central Zone kuchukuliwa
usiku wa jana (Jumatano) wakati walipokuwa studio ya Tongwe Records na
kupelekwa sehemu isiyojulikana, kimewaumiaza wengi. Zitto Kabwe na Nay
wa Mitego ni miongoni mwa walioumizwa na tukio hilo.
Wawili hao wamekilaani kitendo hicho kupitia mitandao tofauti
tofauti. “Uvamizi wa studio ya Tongwe na kumkamata msanii Roma Mkatoliki
ni mwendelezo wa uongozi wa kigangstar na lazima kulaani Kwa nguvu zetu
zote,” ameandika Zitto kwenye Twitter yake.
Naye Nay kupitia mtandao wa Insytagram ameandika, “Kuvamia Ofisi Za watu, heh.! Kumbe nayo ni Kazi.?! Nina Imani uko salama mwanangu, Kamanda @roma2030 Sina ata chembe ya wasi wasi. #Wapo .”
Watu hao wanadaiwa kuwachukuwa vijana wengine wawili waliokuwa katika studio hiyo na wameondoka na computer ya studio na Screen (Tv).

No comments: