Mjue Mwenza kweli
Mjue Mwenza wa
kweli.
Moyo wa mtu ni kama kichaka huwezi
kugundua yalimo ndani yake na siku zote jambo usilo lijua ni sawa na usiku wa
giza na watu wengi tanadanganyika tukifikiri kuwa kila king’aacho ni dhahabu.
Bila shaka u mzima wa afya mpenzi msomaji wa safu hii,usichoke
kumshukuru Mungu ukijaaliwa kuiona siku mpya kwa sababu wapo wengi wanaotamani
kuiona siku mpya lakini hawakuweza kuiona,sio kwamba wao ni wakosefu mbele za
Mungu na wewe ni mwema bali ni kwa neema na mapenzi yake yeye aliye muweza wa
yote Mshukuru kwa kila jamabo.
leo katika safu
hii nakuletea mada inayoitwa Mjue Mwenza wa Kweli,nimekuletea mada hii kwasababu najua unapata ugumu kiasi
gani kumtambua mwenza bora ususani kwa karne hii ambapo utapeli umeshamiri
katika uhusiano,sio wanawake sio wanaume wote wemekuwa hawaaminiani katika
suala la kukabidhiana zawadi nzuri ya Upendo.
Inawezekana upo katika uhusiano na tapeli wa mapenzi bila kujua, au una
mpango wa kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na mtu bila kujua kama ni Tapeli hiyo
ni hatari, unachotakiwa kufanya sasa ni kuanza kumchunguza mpenzi wako mapema
usije kujuta badae kwani wahenga walisema majuto ni mjukuu.
Kumbuka, kuwa katika uhusiano na mtu ambaye haeleweki ni sawa na kukaribisha matatizo katika maisha yako, huna sababu ya kuishi kwa wasiwasi ukiwa hujui mpenzi wako anakuchukulia vipi.
Mpendwa msomaji wa safu ya Mwenza Wa Nani zifuatazo ni sifa za
Mwenza bora,zisome na uzielewe kwa makini kuepusha migogoro ya kimapenzi hasa
unapoanzisha uhusiano na mtu asiye sahihi ‘wrong
person’ wenzetu wanasema.
1. Atataka kukutambulisha kwa
rafiki zake.
Hii ni kati ya alama ya mwenza bora,atakuwa mtu wa kujivunia kuwa na
wewe kila sehemu kwa marafiki zake na hatosita kukutambulisha kwa watu wake wa
karibu.
2. Sio msiri.
Hii ni alama nyingine aliyonayo mwenza bora.Siku zote atakushirikisha
kwenye mambo yake ata kama ni ya kifamilia au kiofisi hatoweza kukuficha.
3.Atakuheshimu.
Mwenza wa kweli atauheshimu na pia ataheshimu mawazo na maamuzi
yako,hawezi kufanya kitu ambacho kitakuudhi wala kukushushia heshima yako kwa
namna moja au nyingine.
4.Atapenda
kuzungumzia malengo.
Mwenza wa kweli atazungumzia malengo ya uhusiano wenu,na atapenda
kutengeneza mwongozo mapenzi yenu pia atakuuliza malengo yako na vitu muhimu unavyovitarajia katika
uhusiano wenu.
5.Atataka ndugu wafahamiane.
Mapenzi hayaishii kwa nyie wawili
pekee bali hata kwa ndugu zenu. Mnapojuana inakuwa rahisi kusaidiana hata
katika mambo mengine ya kawaida.Hivyo mwenza wa kweli atataka ndugu wa pande
zote mbili wafahamiane na waungane kupitia uhusiano wenu.
itandeea.............
No comments: