.

.

"Sikukata tamaa licha ya kuwa msanii mwenye Gundu miaka mingi"- Jay Moe

JAY MOE
 
Mwanamuziki mkongongwe Jay moe amesema hajawahi kukata tama wala kuacha kuzidi kusonga mbele katika safari yake ya muziki licha ya kuambia ana Gundu na hana bahati.

Rapa huyo ambaye anatamba na "singo" yake ya Nisaidie kushare ambapo ujio wake mpya alikuja na ngoma ya Pesa ya madafu,amekuwa kwenye game takribani miaka 17 na sasa ndo anaanza kupata mafanikio ya muziki wake.

Jay moe ameyasema hayo alipokuwa akihojiwa katika kituo cha television cha TBC na kuzidi kuwapa moyo wasanii ambao bado hawajapata mafanikio  katika kile ambacho wanakiamini kutokata tamaa na kuzidi kufanya vizuri zaidi kwenye muziki ambao wanaufanya.

Jay Moe hapo nyuma aliwahi kutamba na vibao kama Mvua na jua,story tatu,so famous na nyingine nyingi ambazo zilifanya vizuri kwa kipindi hicho.

No comments:

Powered by Blogger.