Watu wavamia studio za Tongwe na kumteka Roma na Moni Central Zone
Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule aka Professor Jay, amesema rapper Roma
Mkatoliki pamoja na rapper Moni Central Zone wamechukuliwa na kupelekwa
kusikojulikana na watu waliozivamia studio za Tongwe Records jana
usiku.
Profesa amedai watu hao wamemchukua pia kijana wa kazi, computer ya studio pamoja na TV.
Hii ni taarifa yake:

Hii ni taarifa yake:
ROMA MKATOLIKI AMEKAMATWA USIKU HUU… Nimestushwa sana kusikia kuwa kuna watu wamevamia studio za TONGWE RECORDS majira ya saa moja usiku na wamemchukua ROMA @roma2030 , MONI @moni_centrozone na kijana wa Kazi na pia wamechukua COMPUTER ya studio na Screen (Tv) na wameondoka navyo kusikojulikana.. Mpaka sasa hatujui wamewapeleka wapi!!
No comments: