.

.

Jah Prayzah: Nimeruhusiwa na jeshi la Zimbabwe kuvaa sare zao

 Staa wa Zimbabwe, Jah Prayzah, ameruhusiwa na jeshi la nchini humo kuvaa sare zake popote anapotaka. Mara nyingi muimbaji huyo wa Watora Mari huvaa sare za jeshi wakati akitumbuiza na kwenye mizunguko ya kawaida.

Amesema kuwa kabla ya kuwa mwanamuziki maarufu, alikuwa akipenda mno kuwa mwanajeshi lakini haku fanikiwa. Hata hivyo kama bahati jeshi hilo lilimteua kama balozi wake na kupata ruhusu ya kuvaa nguo zake.
“Kwangu ni moja ya mafanikio makubwa,” amesema. “Siku zote nilikuwa nataka kuwa mmoja wao, hivyo waliponitangaza kuwa balozi wa jeshi la ulinzi nilifurahi sana.” Jah amesema sare hizo hupewa na jeshi lenyewe na zingine hununua mwenyewe anapoenda katika nchi za nje.

 Amedai kuwa zipo sare ambazo huzivaa katika shughuli zake na zingine huzivaa kwenye shughuli maalum za jeshi hilo. Staa huyo alikuwa Tanzania wiki iliyopita ambapo alikuja kushoot video ya wimbo alioshirikishwa na Harmonize.

No comments:

Powered by Blogger.