.

.

Hashtag ya #Dubai Instagram yampa Ommy Dimpoz deal la mamilioni

Ommy Dimpoz aliishi Dubai kwa kula bata kama mwana mfalme kwa kipindi cha mwezi mzima, thanks kwa matumizi yake mazuri ya hashtag kwenye picha zake za Instagram.


Muimbaji huyo wa Cheche amesema kuwa alipoenda Dubai, alipost picha na kuweka hashtag #Dubai. Anasema baada ya muda mfupi, alipokea email kutoka kwa ofisi ya bodi ya utalii nchini humo iliyopenda ifanye naye kazi baada ya kubaini kuwa picha yake ina interaction kubwa na pia akaunti yake ikiwa verified na followers wengi, ikimaanisha kuwa ni mtu maarufu.
Kwenye email ambayo alinionesha, bodi hiyo ilimweleza kuhusu kumpa ofa ya kumzungusha katika vivutio muhimu vya utalii mjini humo bure.

 Anasema baada ya kukutana nao, Ommy aliwatajia kiwango anachotaka kulipwa na baada ya kukubaliana kazi ilianza na kutakiwa kuwema hashtag #MyDubai na #VisitDubai kila alipopost picha Instagram.
“Lakini watu wanajiuliza Ommy amepata wapi mahela ya kwenda kufanya helikopta tour in Dubai,” amesema staa huyo.
“Watu wengine walikuwa wakihesababu kwamba bata lakini mimi pale nilikuwa kwenye kazi. Mfano, ntakupa hiyo tumeenda dinner Burj Khalifa, ukiacha hela ambazo walikuwa wananipa, nilipewa gari ya kutembelea kokote ninapotaka kwenda,” amesema. Ameongeza pia kuwa siku hiyo, yeye na rafiki zake wakiwemo watoto wa Jakaya Kikwete walipewa coupon yenye thamani ya $500 kila mmoja kula bata kwenye jengo hilo refu zaidi duniani.
“Ukiangalia hiyo dinner ilicost karibia milioni 5 au sita.”
Amedai kuwa pamoja na kulipwa, sasa anaweza kwenda kufanya video mjini humo bure kabisa

No comments:

Powered by Blogger.