.

.

Hatuabudu sanamu tunaheshimu- Fr. Innocent Bahati Mushi

Kuelekea Ijumaa kuu na sikukuu ya Pasaka Fr.Innocent atoa ufafanuzi kuhusu wakristo kuabudu sanamu.Soma hapa:


JE, WAKATOLIKI TUNAABUDU SAN AMU NA PICHA?
Maswali tunayoulizwa sisi Wakatoliki na watu hasa wa madhehebu mengine na dini nyingine.
·  Je, wakatoliki wanaabudu mti? Je, ibada ya Ijumaa Kuu ina maana gani (hasa ile ya kubusu msalaba)?
·  Mbona imeandikwa "usije ukajifanyia mfano wa sanamu ukaiabudu. Kwa maana mimi Bwana wako sifananishwi na sanamu yoyote au na kitu cho chote kilichotengenezwa na binadamu" (Kut 20:4-5,5:6-10)?
·  Wakatoliki hawapo kinyume na Maandiko Matakatifu kwa picha na sanamu walizonazo majumbani na makanisani mwao?
o Kwa mfano zile za Bikira Maria na Yosefu? Sasa tujibu maswali haya kwa mtindo wa maswali manane.
JE, WAKATOLIKI TUNATUHUMIWA NINI?
Wakatoliki na hata Wakristo wengine tunatuhumiwa kuabudu mti, sanamu na picha. Mashtaka hayo ni maarufu kabisa tena yana umri mkubwa sana.
Kifupi, tunajibu tuhuma hizo kwa kusema kwamba, hatuabudu mti, sanamu wala picha na wala hatupingani na Maandiko Matakatifu kwa kuwa na sanamu au picha majumbani ama makanisani mwetu.
Hata hivyo, watu inawapasa kwanza kuelewa vyema tunachoamini. Hilo ndilo ninalokusudia kulifafanua na kulielewesha katika sehemu hii ya kitabu. Yaani tunataka kukanusha kwamba Kanisa Katoliki linaendesha sanamu ya ibada.
Lakini, ili kuelewa hilo yaeleweke kwanza mambo mawili: tofauti ya kuabudu na kuheshimu, na halafu mambo mawili yaliyo muhimu katika kuabudu. Mara moja tuanze na vipengee hivi.
KUNA TOFAUTI KATI YA KUABUDU NA KUHESHIMU
Anayeabudiwa na mwenye haki ya kuabudiwa ni Mungu peke yake. Huyo ndiye pekee anayeabudiwa (latria au latreia). Zaidi ya hapo hakuna mtu, kiumbe wala kitu kinachoabudiwa.
Mtu au kiumbe au kitu hupewa heshima tu tena kwa viwango maalumu. Bikira Maria, yaani mama wa Bwana wetu Yesu huheshimiwa kwa heshima ya juu (hyperdulia) na chini yake huheshimiwa watakatifu wengine. Hao na vitu wanavyohusika navyo hupewa heshima ya kadiri (dulia). Picha na sanamu kwa kuwa siyo Mungu haviabudiwi, bali vinaheshimiwa tu.
Kwa sababu gani tunamwabudu Mungu peke yake? Tunamwabudu Mungu kwa sababu:
·    Ndiye Muumba wa vitu vyote, vinavyoonekana na visivyoonekana,
·   Ndiye anayevitawala na kuviongoza vyote,
·   Ndiye mwenye Uwezo juu yetu sisi viumbe wote,
·   Ndiye Anayejua yote,
·   Ndiye Aliye Pote kwa ajili yetu,
·   Ndiye Mwanzo na Mwisho (Alfa na Omega) wa kila kitu,
·   Ndiye Mkuu wa Wakuu na Bwana wa mabwana wote.
Na kifupi, tunapomwabudu, sisi tunakiri kwamba ndiye aliyetuumba, nasi
"Ndani yake YEYE tunaishi, tunakwenda, tunajimudu na kuwa na uhai wetu" (rej. Mdo 17:28).
Kwa kufahamu hili, tunajitahidi kutompa mtu ye yote ama kitu cho chote daraja hilo la kuabudiwa, maana hata yeye mwenyewe ametukataza kwa bidii kabisa (rej. Kum 4:15-24,15:42-48). Sisi tuna masikio na hivyo tumesikia.
ii. Mambo mawili muhimu kwa ibada ya sanamu
Ili kujua kinachofanyika katika Kanisa Katoliki, ni sharti kufuatilia na kutafakari kile kinachofundishwa na kusadikiwa na Wakatoliki wenyewe. Si halali kuhuku
Kwa hali halisi, hakuna ibada yo yote ya sanamu katika Kanisa Katoliki, kwa sababu ili ibada ya sanamu iwe kweli kuabudu, lazima kuwepo na mambo mawili muhimu
· Mosi, nia kamili ya kuabudu sanamu inayohusika au zinazohusika na
·  Pili, kuwepo ibada ya dhati.
Hayo mawili yanakosekana kati ya waamini wa Kanisa Katoliki tunapohusiana na sanamu au picha. Basi, Wakatoliki hawaabudu sanamu wala picha. Tunafanya nini basi? Tunaziheshimu tu.
Anayemwabudu mtu au kitu, ni sharti amhesabu yule mtu au ki kitu kama ndicho kinachomwezesha kuishi, kwenda, kujimudu na kuwa na uhai wake" (rej. Mdo 17:28). Sisi hilo hatufanyi.
Makala hii inapatikana kwa kina katika kitabu cha Padre Titus Amigu "Maswali wabandikwayo Wakatoliki" Jipatie Nakala. Nitaendelea na ufafanuzi wa jambo hilo

No comments:

Powered by Blogger.