.

.

“Weusi siyo kama bendi ya Dansi” – Bonta

 
Staa wa Bongo fleva kutoka kundi la Weusi ambalo limekuwa linafanya vizuri leo kupitia kipindi cha XXL ya clouds amezungumza juu ya kutooneka mara kwa mara kundini.
Bonta amesema amekuwa mbali kutokana na  majukumu ambayo yanamfanya awembali kwenye baadhi  ya kazi zinazofanywa na wanakundi ambao ni Joh Makini,Nikki wa pili,na G nako,

Bonta ambaye ndiye CEO wa kampuni ya WEUSI ambayo imesajiliwa kibiashara amesema "Weusi siyo kama bendi ya dansi.Nipo mbali nao kimajukumu thus why nakosekana kwenye kazi nyingi.Mimi ndio CEO wa WEUSI Kampuni tumeweza kuisajili kibiashara na tunaweza tusiwe marafiki kwenye muziki ila ni marafiki kifamilia.Mimi na Joh Makini tumetoka mbali na Lord Eyes"

Bonta amezungumzia pia  ngoma yake mpya,"Ngoma yangu mpya inaitwa Zero inazungumzia juu ya mfumo mzima wa Elimu kuanzia elimu ya msingi hadi Chuo na nimerekodi tangu mwaka jana.Sijazungumzia kuhusu mtu mmoja,imezungumzia mfumo na huu ndio wakati wake."

 






 

No comments:

Powered by Blogger.