WLAC WAANZISHA MABONANZA KUHAMASISHA JAMII KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA
Bonanza hilo, limefunguliwa na mratibu wa WLAC, Abia Richard jijini Dar es Salaam.Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Bonanza hilo uliofanyika Mwembe Yanga,Temek, Abia amesema lengo la kuanzishwakwa bonanza hilo ni kutaka kuwaunganisha watanzania kupambana na vitendo hivyo bya ukatili wa kijinsia.
Amesema, katika kampeni nyingine ambazo wamekuwa wakiendesha, kundi kubwa ambalo limekuwa likihamasika ni wanawake na wasichana kwa hiyo wanaamini kuanzisha kampeni hiyo kutasaidia kuwahamasisha na wanaume.
Ameongeza, kati ya kundi linalotajwa katika kutenda vitendo vya ukatili wa kijinsia na wanaume pia wamo, lakini katika kampeni nyingi zinazoendeshwa za kuhamasisha kupambana na vitendo hivi, kundi la wanaume wamekuwa wakijiweka pembeni.
" Tunaamini katika kampeni hii kupitia bonanza, wanaume watashiriki kwa wingi kwa sababu wanapenda michezo,” amesema Abia.Ameongeza kuwa, vitendo vya ukatili wa kijinsia vinapaswa kupambanwa na kila mtu katika jamii kwa kuwa vinaathiri sana jamii yetu. Wanaume hawapaswi kukaa pembeni, tunawaomba kupitia michezo hii nao washiriki kupambana navyo.
Katika kampeni hiyo michezo mbalimbali imepangwa, kuwamp ikiwemo ya mpira wa miguu, pete, na mingine mingi, itakayowapa fursa na wanaume kushiriki.
No comments: